Binafsi huwa Sitaman kuwajibu watu Kama huyu, Wanaotoa tuhuma kama hizi wakidhani ni hoja za msingi Kwao. Bila kufahamu ya kuwa, Kabla mtu mwenye Akili timamu hajachukua Hatua ya kuziamini propaganda zao, kitu Cha kwanza mtu huyu huishirikisha Akili yake. Leo Ngoja nipoteze Dakika kadhaa hapa Kwa faida ya wengi. Twende Kwa Mfumo wa Maswali; hivi tuhuma za mauaji ya hawa Viongozi; Moringe Sokoine na Mchungaji Mtikila ( Mwenyezi MUNGU Awarehemu ), Kwa Mbinu ileile ya Ajali za mchongo iliyozoeleka Nchini! Vipi na wao waliutaka Uenyekiti CHADEMA? Pichani; Juu ni Gari Ambalo Mchungaji Mtikila alipata nalo Ajali na Chini ni Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Nchi, Moringe Sokoine. Vipi Kuhusu Marehemu Amina Chifupa( Mwenyezi MUNGU amrehemu ), Kijana wa Miaka 26, anayesemekana Kuuawa na Wauzaji na Wabwia Unga wa CCM(wenzie), Vipi na Yeye Aliutaka UenyekitCHADEMA? Amina Chifupa (1981-2007) Aliyekuwa Mbunge Viti Maalum Jimbo la Mbinga Magharibi. Andiko la miongoni mwa waadishi binafsi, Ndugu Vitali...