WATANZANIA NA WANACHAMA(CDM) MNAHITAJI FREEMAN A. MBOWE AFANYE LIPI ZAIDI YA HILI?

Anaandika; MMM, Martin Maranja Masese(Mtikila)Mhariri; Adv. Dedan Chacha Wangwe.


Pichani; Juu ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania, Mhe. Freeman A. Mbowe. Chini ni Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama pinzani (AZIMIO) Kenya, Mhe. Raila Odinga



Martin Maranja Masese(Mtikila), Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa(Political Analyst) Nchini Tanzania na Mwanacha wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Pichani; MWANDISHI, Martin Maranja Masese(Mtikila), Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa(Political Analyst) Nchini Tanzania, na Mwanacha wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Pichani; MHARIRI, Adv. Dedan Chacha Wangwe, Mwanasheria,  Mwanaharakati wa Masuala ya Kisiasa na Haki za Binadamu Nchi Tanzania. Mwanachama Wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).


RAILA ODINGA A.K.A BABA, ni alama ya ushindi kwa wafuasi wake. Ana wafuasi Wengi na wanampenda na kumuunga mkono.

Pichani; Raila Odinga na Wafuasi wake.

ODINGA kafanikiwa kutengeneza uaminifu mkubwa kwa wafuasi wake. Mwaka 2010 aliitisha maandamano kila Jumatatu hadi wakapata katiba mpya.

Mhe. Raila Odinga(Baba) Katika Maandamano ya Kudai Katiba Mpya.

Huwezi kumkamata RAILA ODINGA Kinyume cha Sheria na kumpa kesi ya ugaidi halafu nchi ya Kenya ikabaki salama. Hii ni Kutokana na Umoja na Ujasiri wa Wanachama na wafuasi wake Wasioruhusu hata chembe ya Uonevu wa Serikali na Chama Tawala dhidi ya Viongozi wao. 

Muda wote, viongozi wenzake waandamizi, wapo naye, hawamuachi, iwe kwenye mikutano au maandamano. Kamwe huwezi kumkuta kiongozi ndani ya Chama Cha ODM na Sasa AZIMIO, amesimama popote anamdhihaki RAILA ODINGA. Wanamheshimu, na Wanautambua Mchango wake Ndani ya Chama na Taifa lao. 

Pichani; Raisi Mtaafu Mhe. Uhuru Kenyatta (kushoto), Akifuatiwa na Mhe. Raila Odinga na Viongozi wengine wa AZIMIO.

Si Serikali, Chama Tawala, Wala Mtu yeyote anayeweza kuharibu mali za ODINGA Kwa Makusudi ya kumkomoa na bado akabaki salama. Mfano; Kuharibu hoteli, Mashamba yake nk. Thubutu! 


Tukirudi Upande wetu Tanzania, hebu tumtizame Kiongozi wa Chama kikuu Cha Upinza(CHADEMA), Mhe. Freeman A. Mbowe;

FREEMAN MBOWE, Wapo viongozi wake waandamizi ambao ndiyo wanashiriki kumdhihaki kwamba kalamba asali!

Pichani; Mhe. Freeman Mbowe

Hebu Tukumbushane hapa Kwa Ufupi;

FREEMAN MBOWE aliitisha maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, Ulioibiwa waziwazi, lakini sisi kama Wanachama na Wananchi hatukujitokeza Kumuunga mkono. Mwisho, wakati wa maandalizi ya Maandamano hayo akakamatwa na Polisi pamoja na wenzake (Mhe. Godbless Lema, Mhe. Boniface Jacob Nk.) wakafichwa kwa siku kadhaa na pengine wangeweza Kuuwawa kimya kimya. lakini Wananchi hatukujitokeza hata Kuudai Uhuru wao.

Pichani; Mhe. Godbless Lema, Chini ni Mhe. Boniface Jacob. 

Februari  Mwaka 2018 Katika Maandamano ya Amani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jijini Dar es Salaam,  Polisi walivuruga maandamano hayo Kwa kutumia Risasi za Moto na hatimaye Walimpiga risasi ya kichwa na Kumuua Binti Mdogo Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Usafirishaji (NIT), Aliyekuwa katika Shughuli zake binafsi Aliyetambulika Kwa majina Akwilina Akwilini Bafta. 

Pichani; Akwilina Akwilini Bafta (1996 - 2018).

Ajabu zaidi, Kesi ya mauaji ya Akwilina akapewa Freeman Mbowe na Viongozi wenzake, Wakashitakiwa na Kuhuhukumiwa Kwa Kesi hiyo. Freeman Mbowe alikamatwa Mwaka 2019 na kuwekwa gerezani miezi 04. Alihukumiwa kifungo gerezani au faini TSH.350M

Pichani; Mhe. John Mnyika, katibu Mkuu CDM(wa kwanza Kushoto) Akifuatiwa na Mhe. Freeman Mbowe wakiwa Mahakamani.


FREEMAN MBOWE, Mwaka 2021, Alikamatwa Kinyume cha Sheria za Nchi akiwa katika Harakati za Kutoa Elimu na Kujenga Uelewa Juu ya Suala la Katiba Mpya Kwa Wananchi Jijini Mwanza. akapewa kesi Bandia ya ugaidi. Kinachosikitisha Wanachama na Taifa Kwa Ujumla Likakaa kimya.

Pichani; Mhe. Freeman Mbowe Mkutanoni.

FREEMAN MBOWE amekaa gerezani miezi nane (08). Na nchi ikatulia tulii! Hata sisi wenzake tuliingiwa na Ubaridi. Wengine walichoka hata kwenda Mahakamani kwenye kesi yake. Wengine ndiyo kabisa hatukuwahi kufika kumuona gerezani au hata Mahakamani kusikiliza kesi yake ya Ugaidi. Tulisubiri kusoma tweets za mrejesho tu. 

FREEMAN MBOWE anapitishwa barabara ya Mandela kila siku asubuhi na Jioni kwenda gerezani Segerea na kupelekwa Mahakamani Sinza. Akichungulia dirishani, anaona Shughuli za watu zinaendelea na hakuna ambaye anajali. Kila kitu kipo kama alivyokiacha.

Pichani; Mhe. Freeman Mbowe Ndani ya Gari la Magereza.

Walevi wanalewa, vijana wanacheza pool table. Daladala zinapiga Safari (route) zake. Hoteli zimefunguliwa Kama kawaida na Hakuna ambacho kimesimama.

FREEMAN MBOWE amekutwa na kesi ya kujibu, kwa kesi Ile ya uongo ya Ugaidi ambayo wengine waliamua kuirusha mubashara ili muuone uongo Ule. Lakini Bado watu tulitulia tulii. Hii ni sababu nyingine kubwa ya kwanini namuunga mkono FREEMAN MBOWE kwa njia hii ambayo ameamua kuichagua sasa (Maridhiano). Yaani, Kwenda mezani kuona labda tutapata Suluhisho la Matatizo ya Taifa hili. Kwasababu ni dhahiri Wananchi Hatuwezi kuandamana, Tunaogopa kupambana na polisi, Tunaogopa maji ya kuwasha na mabomu ya machozi.

Pichani; Mhe. Freeman Mbowe (Kushoto) Akiwa na Mhe. Raila Odinga (Kulia).


Kinacho Shangaza zaidi, Pamoja na Wananchi Kushindwa na kuyaogopa yote hayo, Lakini bado tunalalamika kwanini FREEMAN MBOWE Kaamua Kuchagua Njia ya kukaa mezani Kujadiliana na CCM pamoja na serikali yake Ili Mwananchi wa kawaida aondokane na Uonevu na Ukandamizwaji wa haki zake za msingi, tupate Usawa wa Fursa za Kiuchumi, Kudhibiti wizi na Matumizi mabaya ya Rasilimali na Kodi za Wananchi, Tupate Uhuru wa kweli Nk.  Je, Tunahitaji Afanye Nini Zaidi ya Hili la Sasa?

Yawezekana Hatufaham tunahitaji Nini!

Pichani; Kuanzia Kulia ni Mhe. Jakaya Kikwete(Raisi Mstafu awamu ya nne), Mhe. K. Majaliwa( Waziri Mkuu), Mhe. Freeman Mbowe(Mwenyekiti CHADEMA TAIFA) Mhe. A. Kinana(Makamu Mwenyekiti CCM TAIFA).

Hatutaki Freeman Mbowe akae mezani na CCM na serikali kujadili na kurekebisha masuala kadhaa ya kisiasa, Kiuchumi nk. Sasa tunataka nini? Kama ni Maandaman! Mbona Yale ya November 2020 Hutukuandamana alipotuita tumsaidie kuyapinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020?

Watanzania Tujitafakari Kwa kina, Ili tutambue tunahitaji Nini. Kinyume na Hilo Tutaendelea kulalamika huku tukiyashudia Maovu ya CCM na Serikali yake yakiendelea.


Comments

Popular posts from this blog

NAFASI YA MWENYEKITI CHADEMA(TAIFA) NA TUHUMA ZA CCM