NAFASI YA MWENYEKITI CHADEMA(TAIFA) NA TUHUMA ZA CCM
Vipi Kuhusu Marehemu Amina Chifupa(Mwenyezi MUNGU amrehemu), Kijana wa Miaka 26, anayesemekana Kuuawa na Wauzaji na Wabwia Unga wa CCM(wenzie), Vipi na Yeye Aliutaka UenyekitCHADEMA?
Marehemu Alphonse Mawazo (Mwenyezi MUNGU Amrehemu), aliyeuawa hadharani na Wana CCM. vipi na yeye Aliutaka Uenyekiti?
Vipi kuhusu ndugu Ben Saanane, Bwana Azory Gwanda na wengine wengi ambao wamepotezwa baada ya kuibua au kupinga uchafu wa Utawala au Watawala wa CCM.! Hakika naona na wao waliutaka Uenyekiti CHADEMA Si ndio?
Hoja ya Uenyekiti ndani ya CHADEMA kwenu(CCM) nd’o imekuwa Ajenda ya Miaka mingi. Napata mashaka kwanini nafasi hii Hususani ngazi ya Taifa nd’o ionekane tatizo kwenu.! Mbona katika ngazi za Chini Viongozi tupo tuliodumu katika nafasi zetu Kwa miaka mingi sana Kwa mujibu wa Katiba ya Chama. Lakini mbona hilo kwenu halionekani Kuwa tatizo?
Ieleweke vyema, hiki Chama(CHADEMA) kinafuata Misingi ya Kidemokrasia, na Nguvu ya kura za wanachama zinazopigwa Kwa Uwazi, ndizo zinazoamua nani awepo katika nafasi gani, na Kwa muda gani.
Huku(CHADEMA) nafasi za Uongozi hususani Nafasi ya Mwenyekiti, hatupeani kama Njugu au Pipi kama huko Kwenu(CCM). Mtu yeyote anayestahili na Mwenye vigezo lazima ipigiwe kura na Wanachama na si vinginevyo.
Lakini pia, swali la kujiuliza ni kwanini Mauaji au majaribio yote ya utekaji ambayo CCM na Serikali yake inashutumiwa Kuhusika, Vyombo vya Ulinzi na Usalama Huwa havichukui Hatua yoyote na mambo hayo Huachwa yapite bila kupatiwa Ufumbuzi?
Yawezekana Tuhuma zenu Kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe, Freeman Mbowe zikawa kweli au Uongo! Lakini Cha kujiuliza, Kwa Namna ambayo CCM na Serikali yake inavyoteswa na Suala la Mwenyekiti kuendelea kuwepo katika nafasi hii, Ambayo Anaipata Kwa Kuchaguliwa Kwa Mujibu wa Katiba ya Chama. Na Kwa Namna CCM wanavyotamani kumpoteza hata Kwa kumsweka Gerezani kama walivyojaribu Kwa tuhuma za Ugaidi bandia! Je, wangeshindwa kuzitumia tuhuma hizi za wazi na Nguvu ya dola waliyonayo kumwangusha Kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe? Sidhani na Sina Hakika kama wangeishia kuzisambaza tuhuma hizi, tena Kwa kuwatumia watu wa ndani na nje ya CHADEMA, Hususani wasaka fursa binafsi.
Pia Hakuna Asiyeutambua Ushetani Uliopo ndani ya CCM, Mpo tayari KUWAUA wote wanaoonekana miba au vikwazo Mbele ya Maslahi yenu. Ni Kheri CHADEMA ambayo huwafukuza Uanachama wale wanaokiuka Katiba ya Chama Kwa Makusudi, Wasaliti, na wale wote wanao fikiri au kuamini kuwa Siasa ni Sehemu ya wao kujitengenezea Fursa ya kuupata mkate wao binafsi na Si kuichukulia Siasa kama Chombo cha kuwatumikia Wananchi na Taifa Kwa Ujumla. Kuliko huko CCM ambako Suluhisho la kuukimbia Ukweli, Uwajibikaj na Kulinda Maslahi ya wachache, ni Kuwaua wapinga Udhalimu. Na bila Haya(Aibu) hamzifuati hata Sera za Ujamaa bandia mnaojinasibu nao katika Katiba ya Chama chenu.
Hivi ni nani awezaye Kumpora jamaa yake Haki na Uhuru wake? Ni nani awezaye kuyakataa Mabadliko ya Sheria na mfumo wa Utawala unaowakandamiza jamaa zake? Basi kama ni ujamaa, Mnapaswa kujua CHADEMA ni Wajamaa Zaidi yenu(CCM), kwa kuwa Wakati wote tumekuwa tukisimamia kile kilicho bora kwa ajili ya Jamaa zetu (Watanzania).
Mwisho; Tambuaeni 99% ya WanaCCM pia hampo salama, na hata ndani ya CCM Wapo wahanga wengi sana. Hivi Mnayakumbuka yale yalo mkuta Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kingwangala, Baada ya Kuoneka Mwiba kwenye Maslahi ya Wenzie(WanaCCM)? Ni MUNGU tu mpaka Leo bado tupo nae.
Sasa nyie Watanzania mlioamua Kutumika vibaya ili wachache waendelee kunufaika na nyie kupoozwa njaa zenu kwa Muda mfupi, huku Mkiendelea kutengeneza njaa Kali na ya Kudumu juu ya vizazi vyenu; Endeleeni, Kwa Maana Apendezwae na Maovu, Naye ni MWOVU zaidi.
Hivyo Niwaombe wote wenye Utimamu wa Akili, tumieni Akili na Uelewa wenu kupima mambo Kabla ya kuyaamini.
Pia kipekee, niitumie nafasi hii, Kuwashukuru wale wote mnaojitolea katika kupinga Maovu Kwa Namna mbali mbali Hapa nchini, Namwomba Mwenyezi MUNGU awaridhia Duniani na Akhera pia.
#No_Hate_No_Fear ✌🏼
#KatibaBoraUstawiWaTaifa
Comments
Post a Comment